Tetesi za soka Ijumaa 27.07.2018: Perisic, Martial, Alderweireld, Vida, Morata
Manchester United bado ina matumaini kusaini mkataba na winga wa Milan Ivan Perisic mwenye umri wa miaka 29 na itamuuza tu mshambuliaji wa Ufaransa Anthony Martial, mwenye umri wa miaka 22, ikiwa mchezaji huyo wa Croatian atapatikana. (Mirror)

Mlinzi wa Tottenham raia wa Ubelgiji Toby Alderweireld, mwenye umri wa miaka 29, amesalia kuwa ndiye anayepewa kipaumbele kusaini mkataba na Manchester United lakini the Londoners wanataka £55m au Anthony Martial ajumuishwe katika mazungumzo ya mkataba. (Independent)

Mmiliki wa Spurs Daniel Levy anaamini kuwa anaweza kusaini mkataba na mchezaji wa safu ya kati wa Aston Villa Muingereza Jack Grealish, mwenye umri wa miaka 22, kwa £20m. (Mirror)
Liverpool hawana nia ya kusaini mkataba na mlinzi wa Besiktas Domagoj Vida, mwenye umri wa miaka 29,licha ya kuwa na uhusiano na timu ya taifa ya Croatia. (Liverpool Echo)
Chelsea imeiambia AC Milan ilipe hadi £62m ikiwa wanataka kusaini mkataba na mshambuliaji Muhispania Alvaro Morata mwenye umri wa miaka 25. (Sky Sports)

Maafisa wa Chelsea wamesafiri hadi Italia kusaini mkataba na mlinzi wa Juventus Daniele Rugani, mwenye umri wa miaka 23, lakini wanasitasita kutimiza kiwango cha thamani yake cha £40m (Times - subscription required)
Mmiliki wa Blues Roman Abramovich na mkurugenzi Marina Granovskaia watakutana mjini Nice kushauriana kuhusu malengo yao ya uhamisho wa wachezaji (Evening Standard)
Barcelona wako tayari kukubali pendekezo la Everton la kiwango cha £27m kumnunua mlinzi wa timu ya taifa ya Colombia Yerry Mina, mwenye umri wa miaka 23. (Goal)

Mchezaji wa Everton wa safu ya kati Muholanzi Davy Klaassen, mwenye umri wa miaka 25, anazungumza na Werder Bremen juu ya hatua ya kumnunua kwa zaidi ya £13m . (Liverpool Echo)
Crystal Palace na Everton wana azma ya kusaini mktaba na mchezaji wa kiungo cha kati wa Roma mwenye umri wa miaka 27 Mfaransa French Maxime Gonalons kwa £10m. (Evening Standard)
West Ham wanaangalia uwezekano wa kumchukua mchezaji wa zamani wa kiungo cha kati wa Paris Saint-Germain Mfaransa Hatem Ben Arfa, mwenye umri wa miaka 31, kwa bila malipo. (Foot365 via Sports Mole)
Mchezaji wa safi ya mashambulizi wa Arsenal na Ufaransa Thierry Henry anachunguzwa kwa ajili ya fursa ya kuchukua nafasi ya meneja baada ya Aston Villa kuamua kusalia na Steve Bruce kama mkuu wake. (Mirror)

Brighton wanakaribia kusaini mkataba na mchezaji wa safu ya mashambulizi raia wa Ecuador Billy Arce mwenye umri wa miaka 20 kutoka timu ya Independiente del Valle. (Diario Expreso via Sport Witness)
Fenerbahce inataka kumchukua mlinzi wa Stoke Muholanzi Bruno Martins Indi, mwenye umri wa miaka 26, kwa mkataba wa deni la msimu. (Takvim - in Turkish)

Derby wako tayari kumuuza Mshambuliaji wa Czech Matej Vydra, mwenye umri wa miaka 26, kwa Leedskatika mkataba wa £11m, na watatumia pesa kumnunua mshambuliaji wa Ipswich Muingereza Martyn Waghorn mwenye umri wa miaka 28 (Sun)
Blackburn watasaini mkataba na mchezaji wa safu ya kati wa Chelsea Muingereza Kasey Palmer, akiwa na umri wa 21, kwa deni hadi mwishoni mwa mwaka huu . (Sky Sports)
Rangers wataangalia uwezekano wa kusaini mkataba na mchezaji wa safu ya kati Muingereza Kean Bryan, mwenye umri wa miaka 21 anayechezea Manchester City , ikiwa mchezaji wa safu ya kati wa Uingereza Josh Windass, mwenye umri wa miaka 24, ataondoka Ibrox. (Mail)
No comments:
Post a Comment