Kupatwa huko hutokea wakati mwezi unapoingia katika kivuli cha dunia.
Katika awamu tofauti kupatwa huko kwa mwezi kutafanyika kwa saa tatu na dakika 55.
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionUsiku wa kupatwa kwa mwezi hushirikishwa na uzushi wa kuwepo kwa 'mwezi wa damu' kutokana na rangi yake nyekundu.
Kwa nini unaitwa 'mwezi wa damu'?
Usiku wa kupatwa kwa mwezi hushirikishwa na dhana na wa kuwepo kwa 'mwezi wa damu' kutokana na rangi yake nyekundu.
Hilo linatokana na athari za kutazama miale ya jua katika anga na rangi za machungwa na nyekundu zinazoonekana katika mwezi.
Wakati huohuo , wakati wa kupatwa kwa mwezi mnamo tarehe 27 Julai, mwezi utakuwa mbali na zaidi kutoka kwa dunia.
Kupatwa kwa mwezi mnamo tarehe 27 Julai kutaonekana Ulaya, Afrika, mashariki ya kati , katikati mwa Asia na Australia ikiwa ni maeneo yote isipokuwa kaskazini mwa Marekani.
Hautalazimika kutumia darubini kuutazama mwezi huo.
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionKivuli cha tukio hilo kitaonekana katika setlait bila kuziba mwangaza wote. Nchini Uingereza hautaweza kuona mwanzo wa tukio hilo
Nani atakayeuona vizuri zaidi?
Eneo zuri la kulitazama tukio hilo ni eneo nusu ya Mashariki mwa Afrika ,Mashariki ya kati na katikati mwa bara Asia.
Tukio hilo halitaonekana katika maeneo ya kati na Marekani Kaskazini.
Kusini mwa Marekani , unaweza kuonekana kiasi katika maeneo ya mashariki hususan miji ya Buenos Aires, Montevideo, Sao Paulo na Rio de Janeiro.
Katika miji mingine ya karibu utaonekana wakati mwezi utakapokuwa ukiondoka katika eneo hilo-huo ni mstari ambao ardhi na anga zinaonekana kukutana.
No comments:
Post a Comment