Sheria ya kikomo cha umri wa kugombea urais yaidhinishwa na mahakama Uganda
Mahakama ya katiba nchini Uganda imeidhinisha mageuzi ya katiba yaliondoa kikomo kwa umri wa kugombea urais.
Majaji wanne kati ya watano wa jopo la majaji wamesema mageuzi hayo hayakiuki katiba, na pia hayendi kinyume na hsri aya muongozo wa bunge nchini.
Awali umri wa mwisho kwa kugombea ilikuwa miaka 75.
- Nini chanzo cha moto mkubwa uliozusha maafa Ugiriki?
- 'Mashujaa' wa vita vya ukeketaji Tanzania
- Uganda yaondoa kikomo cha umri wa kugombea urais
Hii ina maana Rais wa nchi hiyo Yoweri Kaguta Museveni atakua huru kugombea katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2021.
Kikao cha kutoa uamuzi huo uliowasilishwa katika mahakama kuu huko Mbale kilianza kwa naibu jaji mkuu, Alfonse Owiny-Dollo, kuanza kwa kuomba radhi kwa mahakama kuchelewa kuanza kwa muda uliopangwa awali.
No comments:
Post a Comment